1 Wakorintho 4:19
Lakini, Bwana akipenda, nitakuja kwenu upesi; na hapo ndipo nitakapojionea mwenyewe, sio tu kile wanachoweza kusema hao wenye majivuno, bali pia kila wanachoweza kufanya.
Biblia Takatifu
In The King James Version
In Context
18Baadhi yenu wameanza kuwa na majivuno wakidhani kwamba sitakuja tena kwenu.
20Maana Utawala wa Mungu si shauri la maneno matupu, bali ni nguvu.
Cross References
Acts 18:21Bali alipokuwa anaondoka, alisema, “Mungu akipenda nitakuja kwenu tena.” Akaondoka Efeso kwa meli.
Acts 20:2Alipitia sehemu za nchi zile akiwatia watu moyo kwa maneno mengi. Halafu akafika Ugiriki.
1 Corinthians 2:6Hata hivyo, sisi tunatumia lugha ya hekima kwa wale waliokomaa kiroho; lakini hekima hiyo si ya hapa duniani, wala si ya watawala wa dunia hii ambao wako katika mkumbo wa kupotea.
1 Corinthians 11:34Na kama kuna yeyote aliye na njaa, na ale nyumbani kwake, ili kukutana kwenu kusisababishe hukumu. Lakini, kuhusu yale mambo mengine, nitawapeni maelezo nitakapokuja.
1 Corinthians 16:5Nitakuja kwenu, baada ya kupitia Makedonia—maana nataraji kupitia Makedonia.
2 Corinthians 1:23Mungu ndiye shahidi wangu—yeye anajua moyo wangu! Mimi sikuja tena Korintho, kwa sababu tu ya kuwahurumieni.