1 Wafalme 13:2
Akapiga kelele dhidi ya madhabahu kwa neno la Bwana: “Ee madhabahu, madhabahu! Hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Mwana aitwaye Yosia atazaliwa katika nyumba ya Daudi. Juu yako atawatoa dhabihu makuhani wa mahali pa juu pa kuabudia miungu wale ambao wanatoa sadaka hapa sasa, nayo mifupa ya wanadamu itachomwa juu yako.’ ”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 32:1Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitasema; 2 sikia, ee nchi, maneno ya kinywa changu. 1
2 Kings 22:1Yosia alikuwa na miaka minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka thelathini na mmoja. Mama yake aliitwa Yedida binti Adaya, kutoka Boskathi.
2 Kings 23:16Kisha Yosia akatazama huku na huko, naye alipoona makaburi yaliyokuwa huko kwenye kilima, akaamuru mifupa itolewe humo na akaichoma juu ya madhabahu ya Betheli ili kupanajisi. Hili lilitokea kulingana na neno la Bwana lililosemwa na mtu wa Mungu ambaye alitangulia kusema mambo haya.
2 Chronicles 34:4Mbele ya macho yake, wakazibomoa madhabahu za Mabaali, wakazivunja madhabahu za kufukizia uvumba zilizokuwa zimesimama juu yake, wakazivunja nguzo za Ashera, sanamu na vinyago. Hivi alivivunja vipande vipande na kuvisambaza juu ya makaburi ya waliokuwa wamevitolea kafara.
Isaiah 1:2Sikieni, enyi mbingu! Sikilizeni, enyi dunia! 2 Kwa maana Bwana amesema: 1 “Nimewalisha watoto na kuwalea, 2 lakini wameniasi mimi. 1
Isaiah 44:26niyathibitishaye maneno ya watumishi wake, 2 na kutimiza utabiri wa wajumbe wake, 1 “niambiaye Yerusalemu, ‘Itakaliwa na watu,’ 2 niambiaye miji ya Yuda kuwa, ‘Itajengwa,’ 2 na kuhusu magofu yake, ‘Mimi nitayatengeneza,’ 1