1 Timotheo 4:1
Roho asema waziwazi kwamba katika siku za mwisho baadhi ya watu wataiacha imani na kufuata roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 3:13Ndipo Bwana Mungu akamuuliza mwanamke, “Ni nini hili ambalo umelifanya?” Mwanamke akajibu, “Nyoka alinidanganya, nami nikala.”
Deuteronomy 4:30Wakati mnapokuwa katika dhiki, nayo mambo haya yote yamewatokea siku hizo, ndipo mtamrudia Bwana Mungu wenu na kumtii.
1 Kings 22:22“ Bwana akauliza, ‘Kwa njia gani?’ “Akasema, ‘Nitakwenda na kuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.’ “ Bwana akasema, ‘Utafanikiwa katika kumshawishi. Nenda ukafanye hivyo.’
Isaiah 2:2Katika siku za mwisho 1 mlima wa Hekalu la Bwana utaimarishwa 2 kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote, 1 utainuliwa juu ya vilima, 2 na mataifa yote yatamiminika huko.
Jeremiah 49:39“Lakini nitarudisha mateka wa Elamu 2 katika siku zijazo,” 4 asema Bwana.
Ezekiel 38:16Utakuja dhidi ya watu wangu Israeli kama wingu lifunikavyo nchi. Siku zijazo, ee Gogu, nitakuleta wewe dhidi ya nchi yangu, ili kwamba mataifa wapate kunijua Mimi nitakapojionyesha mtakatifu kwa kukupitia wewe mbele ya macho yao.