1 Timotheo 4:6
Kama ukiwakumbusha ndugu mambo haya, utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, uliyelelewa katika kweli ya imani na yale mafundisho mazuri uliyoyafuata.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
5kwa sababu kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba. 1 Mtumishi Mwema Wa Yesu Kristo
Cross References
Proverbs 4:2Ninawapa mafundisho ya maana, 2 kwa hiyo msiyaache mafundisho yangu. 1
Matthew 13:52Akawaambia, “Basi kila mwalimu wa sheria aliyefundishwa elimu ya Ufalme wa Mbinguni ni kama mwenye nyumba anayetoa kutoka ghala yake mali mpya na mali ya zamani.” 1 Yesu Akataliwa Nazareti (Marko 6:1-6; Luka 4:16-30)
Acts 20:31Hivyo jilindeni! Kumbukeni kwamba kwa miaka mitatu sikuacha kamwe kuwaonya kila mmoja kwa machozi usiku na mchana.
Romans 15:15Nimewaandikia kwa ujasiri vipengele kadha wa kadha katika waraka huu kama kuwakumbusha tena kwa habari ya ile neema Mungu aliyonipa,
1 Corinthians 4:17Kwa sababu hii ninamtuma Timotheo, mwanangu mpendwa na mwaminifu katika Bwana. Yeye atawakumbusha kuhusu njia za maisha yangu katika Kristo Yesu, ambayo yanakubaliana na mafundisho yangu ninayofundisha katika kila kanisa.
2 Corinthians 6:4Bali kama watumishi wa Mungu tuonyeshe kwa kila njia: katika saburi nyingi; katika dhiki, katika misiba, na katika shida;