2 Chronicles 1:4
Basi Daudi alikuwa amelipandisha Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu mpaka mahali alipokuwa amepatengeneza kwa ajili yake, kwa sababu alikuwa amesimamisha hema kwa ajili ya hilo Sanduku huko Yerusalemu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Samuel 6:2Yeye na watu wake wote wakatoka Baala ya Yuda + 6:2 Baala ya Yuda ni jina la Kiebrania; yaani Kiriath-Yearimu. kulipandisha Sanduku la Mungu kutoka huko, linaloitwa kwa Jina, naam, jina la Bwana Mwenye Nguvu Zote, ambaye anaketi katika kiti cha enzi kati ya makerubi walioko juu ya hilo Sanduku.
1 Chronicles 13:5Basi Daudi akawakusanya Waisraeli wote, kuanzia Mto Shihori ulioko Misri hadi Lebo-Hamathi, ili kulileta Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu.
1 Chronicles 15:3Daudi akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu ili kulipandisha Sanduku la Bwana na kulileta hadi kwenye sehemu aliyokuwa ametengeneza kwa ajili yake.
1 Chronicles 15:25Basi Daudi pamoja na wazee wa Israeli na majemadari wa vikosi vya elfu wakaenda ili kulipandisha Sanduku la Agano la Bwana kutoka nyumba ya Obed-Edomu kwa shangwe.
Psalms 132:5mpaka nitakapompatia Bwana mahali, 2 makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.” 1