2 Nyakati 15:8
Asa aliposikia maneno haya na unabii wa Azaria mwana wa Odedi nabii, akajipa moyo. Akaziondoa sanamu zote zilizokuwa machukizo katika nchi yote ya Yuda na Benyamini na kutoka miji aliyoiteka ya vilima vya Efraimu. Akakarabati madhabahu ya Bwana iliyokuwa mbele ya ukumbi wa Hekalu la Bwana.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 27:15“Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
1 Kings 11:5Solomoni akafuata Ashtorethi mungu mke wa Wasidoni, na Moleki + 11:5 Moleki au Milkomu ni mungu aliyekuwa akiabudiwa na Waamoni; alikuwa chukizo kwa sababu watoto walitolewa kafara kwake. mungu aliyekuwa chukizo la Waamoni.
1 Kings 15:9Katika mwaka wa ishirini wa utawala wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Asa akawa mfalme wa Yuda,
2 Kings 18:22Nawe kama ukiniambia, “Tunamtumainia Bwana Mungu wetu”: je, siyo yeye ambaye Hezekia aliondoa mahali pake pa juu pa kuabudia miungu na madhabahu zake, akiwaambia Yuda na Yerusalemu, “Ni lazima mwabudu mbele ya madhabahu haya katika Yerusalemu”?
2 Chronicles 4:1Mfalme Solomoni akatengeneza madhabahu ya shaba yenye urefu wa dhiraa ishirini, + 4:1 Dhiraa 20 ni sawa na mita 9. upana wa dhiraa ishirini na kimo chake dhiraa kumi. + 4:1 Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5.
2 Chronicles 13:19Abiya akamfuatia Yeroboamu na kuteka miji ya Betheli, Yeshana na Efroni kutoka kwake, pamoja na vijiji vinavyoizunguka miji hiyo.