2 Chronicles 22:11
Lakini Yehosheba, binti wa Mfalme Yehoramu, akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa. Akamweka Yoashi pamoja na yaya wake ndani ya chumba cha kulala. Kwa kuwa Yehosheba, aliyekuwa binti wa Mfalme Yehoramu, na pia alikuwa mke wa kuhani Yehoyada, alikuwa dada yake Ahazia, akamficha huyo mtoto ili Athalia asimuue.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Samuel 7:13Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, nami nitaimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake milele.
2 Kings 11:2Lakini Yehosheba, binti wa Mfalme Yehoramu, aliyekuwa pia dada yake Ahazia, akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa. Akamweka Yoashi pamoja na yaya wake ndani ya chumba cha kulala na kumficha humo ili Athalia asimwone; kwa hiyo hakuuawa.
2 Chronicles 23:1Katika mwaka wa saba, Yehoyada akaonyesha nguvu zake. Alifanya agano na wakuu wa vikosi vya mamia: yaani Azaria mwana wa Yerohamu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri.
Psalms 76:10Hakika ghadhabu yako dhidi ya wanadamu inakuletea sifa, 2 na masalia ya ghadhabu yako unajifunga mshipi. 1
Isaiah 65:8Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Kama vile divai mpya ingali bado inapatikana 2 katika kishada cha zabibu, 1 nao watu husema, ‘Usikiharibu, 2 kwa kuwa bado kuna kitu kizuri ndani yake,’ 1 hivyo ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu; 2 sitawaangamiza wote. 1
Acts 4:28Wao wakafanya yale ambayo uweza wako na mapenzi yako yalikuwa yamekusudia yatokee tangu zamani.