2 Chronicles 32:31
Lakini wakati wajumbe walipotumwa na watawala wa Babeli kumuuliza juu ya ishara ambayo ilitokea katika nchi, Mungu alimwacha ili kumjaribu na kujua kila kitu kilichokuwa moyoni mwake.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 22:1Baadaye Mungu akamjaribu Abrahamu. Akamwambia, “Abrahamu!” Abrahamu akajibu, “Mimi hapa.”
Deuteronomy 8:16Aliwapa mana ya kula jangwani, kitu ambacho baba zenu hawakukijua, ili kuwanyenyekesha na kuwajaribu ninyi ili mwishoni apate kuwatendea mema.
Judges 16:20Yule mwanamke akamwita, “Samsoni, hao Wafilisti wanakujia!” Akaamka toka usingizini akasema, “Nitatoka nje kama hapo awali, nitawakungʼutia mbali na kuwa huru.” Lakini hakujua kuwa Bwana amemwacha.
2 Kings 20:11Ndipo nabii Isaya akamwita Bwana, naye Bwana akakifanya kivuli kurudi nyuma hatua kumi ambazo kilikuwa kimeshuka kwenye ngazi ya Ahazi. 1 Wajumbe Kutoka Babeli (Isaya 39:1-8)
Job 1:11Lakini nyoosha mkono wako na kupiga kila kitu alicho nacho, naye kwa hakika atakulaani mbele za uso wako.”
Psalms 27:9Usinifiche uso wako, 2 usimkatae mtumishi wako kwa hasira; 2 wewe umekuwa msaada wangu. 1 Usinikatae wala usiniache, 2 Ee Mungu Mwokozi wangu. 1