2 Chronicles 9:24
Mwaka baada ya mwaka, kila mmoja ambaye alikuja, alileta zawadi, vyombo vya fedha na dhahabu, majoho, silaha na vikolezi, farasi na nyumbu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Samuel 10:27Lakini baadhi ya watu wakorofi walisema, “Huyu mtu atawezaje kutuokoa?” Wakamdharau na wala hawakumletea zawadi. Lakini Sauli akanyamaza kimya.
1 Kings 10:10Naye akampa mfalme talanta 120 + 10:10 Talanta 120 za dhahabu ni sawa na tani 4.5. za dhahabu, kiasi kikubwa sana cha vikolezi na vito vya thamani. Haikuwahi kamwe kuletwa tena vikolezi vingi hivyo kuletwa kama vile malkia wa Sheba alivyompa Mfalme Solomoni.
2 Chronicles 9:9Naye akampa mfalme talanta 120 + 9:9 Talanta 120 za dhahabu ni sawa na tani 4.5. za dhahabu, kiasi kikubwa cha vikolezi na vito vya thamani. Haikuwahi kamwe kuletwa vikolezi vizuri kama vile Malkia wa Sheba alivyompa Mfalme Solomoni.
Job 42:11Ndipo ndugu zake wote waume kwa wake na kila mtu aliyemfahamu mwanzoni, wakaja wakala pamoja naye katika nyumba yake. Wakamfariji na kumtuliza moyo juu ya taabu yote Bwana aliyoileta juu yake, nao kila mmoja akampa kipande cha fedha na pete ya dhahabu.
Psalms 72:10Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali 2 watamletea kodi; 1 wafalme wa Sheba na Seba 2 watampa zawadi. 1