2 Wakorintho 12:16
Basi, mtakubali kwamba sikuwa mzigo kwenu. Lakini labda mtu mwingine atasema: “Kwa vile Paulo ni mwerevu, amewafanyieni ulaghai.”
Biblia Takatifu
In The King James Version
But be it so, I did not burden you: nevertheless, being crafty, I caught you with guile.
In Context
17Je, mimi niliwanyonyeni kwa njia ya mjumbe yeyote niliyemtuma kwenu?
Cross References
2 Corinthians 1:12Sisi tunajivunia kitu kimoja: dhamiri yetu inatuhakikishia kwamba tumeishi ulimwenguni hapa, na hasa kati yenu, kwa unyenyekevu na unyofu tuliojaliwa na Mungu; hatukuongozwa na hekima ya kibinadamu bali neema ya Mungu.
2 Corinthians 7:2Tunaomba mtupe nafasi mioyoni mwenu! Hatujamkosea mtu yeyote, hatujamdhuru wala kumdanganya mtu yeyote.
2 Corinthians 11:9Nilipokuwa nanyi sikumsumbua mtu yeyote nilipohitaji fedha; ndugu waliotoka Makedonia waliniletea kila kitu nilichohitaji. Nilikuwa mwangalifu sana nisiwe mzigo kwa namna yoyote ile, na nitaendelea kufanya hivyo.
1 Thessalonians 2:3Jambo tunalosisitiza kwenu si jambo linalotegemea uongo au nia mbaya; wala hatupendi kumdanganya mtu yeyote.
1 Peter 2:3Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mmegundua kwamba Bwana ni mwema.”