2 Wakorintho 2:3
Niliandika hivyo kama nilivyofanya, ili nikija nisihuzunishwe na wale watu ambao wangenifanya nifurahi. Nina uhakika na ninyi nyote, kwamba wote mngeshiriki furaha yangu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Corinthians 4:21Ninyi amueni. Je, nije kwenu na fimbo, au nije kwa upendo na kwa roho ya upole?
2 Corinthians 7:6Bali Mungu, yeye awafarijie wenye huzuni, alitufariji kwa kufika kwake Tito.
2 Corinthians 7:12Hivyo ingawa niliwaandikia, haikuwa kwa sababu ya huyo aliyekosa au huyo aliyekosewa. Lakini nilitaka ninyi wenyewe mwone, mbele za Mungu, jinsi mlivyojitoa kwa ajili yetu.
2 Corinthians 12:11Nimekuwa mjinga, lakini ninyi mmenilazimisha niwe hivyo. Kwa kuwa ilinipasa kusifiwa na ninyi, kwa sababu mimi si dhalili kuliko wale “mitume walio bora,” ingawa mimi si kitu.
Galatians 5:10Nina hakika katika Bwana kwamba hamtakuwa na msimamo mwingine. Mtu anayewachanganya anastahili adhabu, hata awe nani.
Philemon 1:21Nikiwa na hakika ya utii wako, nakuandikia, nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya yale ninayokuomba.