2 Samweli 17:16
Sasa tumeni ujumbe haraka na kumwambia Daudi, ‘Usiku huu usilale kwenye vivuko katika jangwa; vuka bila kukosa, la sivyo, mfalme pamoja na watu wote waliofuatana naye watamezwa.’ ”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Samuel 15:14Ndipo Daudi akawaambia maafisa wake wote waliokuwa pamoja naye huko Yerusalemu, “Njooni! Ni lazima tukimbie, la sivyo hakuna hata mmoja wetu atakayeokoka kutoka mkononi mwa Absalomu. Ni lazima tuondoke kwa haraka, la sivyo atakuja mbio na kutupata, atatuangamiza na kuupiga mji kwa upanga.”
2 Samuel 15:35Je, makuhani Sadoki na Abiathari hawatakuwa pamoja nawe? Waambie lolote utakalosikia katika jumba la mfalme.
2 Samuel 20:19Sisi ni watu wa amani na waaminifu katika Israeli. Wewe unajaribu kuharibu mji ambao ni mama katika Israeli. Kwa nini unataka kumeza urithi wa Bwana?”
Psalms 55:8ningaliharakisha kwenda mahali pa salama, 2 mbali na tufani kali na dhoruba.” 1
Psalms 57:3Hutumana kutoka mbinguni na kuniokoa, 2 akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali; 2 Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake. 1
Matthew 24:16basi wale walioko Uyahudi wakimbilie milimani.