2 Samweli 19:32
Basi Barzilai alikuwa mzee sana mwenye umri wa miaka themanini. Alikuwa amempatia mfalme mahitaji wakati alipokuwa anaishi huko Mahanaimu, kwa kuwa alikuwa mtu tajiri sana.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 5:27Methusela aliishi jumla ya miaka 969, ndipo akafa.
Genesis 25:7Kwa jumla, Abrahamu aliishi miaka 175.
Genesis 50:26Kwa hiyo Yosefu akafa akiwa na umri wa miaka 110. Baada ya kumtia dawa ili asioze, akawekwa kwenye jeneza huko Misri.
1 Samuel 25:2Mtu mmoja huko Maoni, aliyekuwa na makao huko Karmeli, alikuwa tajiri sana. Alikuwa na mbuzi elfu moja na kondoo elfu tatu, aliokuwa akiwakata manyoya huko Karmeli.
2 Kings 15:20Menahemu akatoza fedha hizi kwa nguvu kutoka kwa Israeli. Kila mtu tajiri alilazimika kuchanga shekeli hamsini za fedha + 15:20 Shekeli 50 za fedha ni sawa na gramu 600. ambazo alipewa mfalme wa Ashuru. Basi mfalme wa Ashuru akajiondoa na hakuendelea kuikalia nchi.
Psalms 90:3Huwarudisha watu mavumbini, 2 ukisema, “Rudini mavumbini, enyi wanadamu.” 1