2 Samuel 21:10
Rispa binti Aiya akachukua nguo ya gunia, akajitandikia juu ya mwamba. Kuanzia mwanzo wa mavuno mpaka mvua ziliponyesha juu ya miili ya hao waliouawa, Rispa hakuruhusu ndege wa angani kuwagusa wakati wa mchana, wala wanyama wa mwitu wakati wa usiku.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
11Daudi alipoambiwa kile Rispa binti Aiya, suria wa Sauli, alichokuwa amekifanya,
Cross References
Genesis 40:19Katika siku hizi tatu, Farao atakata kichwa chako na kukutundika juu ya mti. Nao ndege watakula nyama ya mwili wako.”
Deuteronomy 21:13avue nguo alizokuwa amevaa alipotekwa. Baada ya kuishi nyumbani mwako na kumwombolezea baba yake na mama yake kwa mwezi mzima, ndipo utakapoweza kumwendea na kuwa mume wake naye atakuwa mke wako.
Deuteronomy 21:23kamwe msiuache mwili wake mtini usiku kucha. Hakikisheni mnauzika mwili wake siku ile ile, kwa sababu kila mtu anayeangikwa mtini yupo chini ya laana ya Mungu. Msiinajisi nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa kama urithi wenu.
2 Samuel 3:7Basi Sauli alikuwa amekuwa na suria, jina lake Rispa binti wa Aiya. Naye Ish-Boshethi akamwambia Abneri, “Kwa nini umekutana kimwili na suria wa baba yangu?”
1 Kings 18:41Eliya akamwambia Ahabu, “Nenda, ukale na kunywa, kwa kuwa kuna sauti ya mvua kubwa.”
Jeremiah 5:24Wao hawaambiani wenyewe, 2 ‘Sisi na tumwogope Bwana Mungu wetu, 1 anayetupatia mvua za masika na za vuli kwa majira yake, 2 anayetuhakikishia majuma ya mavuno kwa utaratibu.’ 1