Acts 10:43
Manabii wote walishuhudia juu yake kwamba kila mtu amwaminiye hupokea msamaha wa dhambi katika Jina lake.” 1 Watu Wa Mataifa Wapokea Roho Mtakatifu
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Jeremiah 31:34Mtu hatamfundisha tena jirani yake, 2 wala mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue Bwana Mungu,’ 1 kwa sababu wote watanijua mimi, 2 tangu aliye mdogo kabisa kwao, hadi aliye mkuu sana,” 4 asema Bwana. 1 “Kwa sababu nitasamehe uovu wao, 2 wala sitazikumbuka dhambi zao tena.”
Micah 7:18Ni nani Mungu kama wewe, 2 ambaye anaachilia dhambi 1 na kusamehe makosa 2 ya mabaki ya urithi wake? 1 Wewe huwi na hasira milele, 2 bali unafurahia kuonyesha rehema. 1
Malachi 4:2Bali kwenu ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mabawa yake. Nanyi mtatoka nje na kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka zizini.
Luke 24:25Yesu akawaambia, “Ninyi ni wajinga kiasi gani, nanyi ni wazito mioyoni mwenu kuamini mambo yote yaliyonenwa na manabii!
John 1:45Filipo naye akamkuta Nathanaeli na kumwambia, “Tumemwona yeye ambaye Mose aliandika habari zake katika Sheria na ambaye pia manabii waliandika kumhusu, yaani, Yesu wa Nazareti, mwana wa Yosefu.”
John 5:24“Amin, amin nawaambia, yeyote anayesikia maneno yangu na kumwamini yeye aliyenituma, anao uzima wa milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini, na kuingia uzimani.