Acts 12:20
Basi Herode Agripa alikuwa amekasirishwa sana na watu wa Tiro na Sidoni. Hivyo watu wa miji hiyo miwili wakaungana pamoja wakatafuta kukutana naye. Wakiisha kuungwa mkono na Blasto, mtumishi maalum wa Mfalme Herode Agripa aliyeaminika, wakaomba mapatano ya amani maana nchi zao zilitegemea nchi ya huyo mfalme kwa mahitaji yao ya chakula.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 10:19na mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.
1 Kings 5:9Watu wangu watayakokota kutoka Lebanoni hadi kwenye bahari, nami nitayafunga mafungu mafungu yaelee juu ya maji hadi utakapoelekeza. Huko nitayatenganisha, nawe utaweza kuyachukua. Wewe utakidhi haja yangu kwa kunipatia chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwangu.”
2 Chronicles 2:15“Sasa basi bwana wangu na awapelekee watumishi wake ngano, shayiri, mafuta ya zeituni na mvinyo kama alivyoahidi,
Proverbs 17:14Kuanzisha ugomvi ni kama kutoboa bwawa la maji; 2 kwa hiyo acha jambo hilo kabla mabishano hayajaanza. 1
Proverbs 25:8usiharakishe kukipeleka mahakamani, 1 maana utafanya nini mwishoni 2 kama jirani yako atakuaibisha? 1
Isaiah 23:1Neno kuhusu Tiro: 1 Ombolezeni, enyi meli za Tarshishi! 2 Kwa kuwa Tiro imeangamizwa, 2 imeachwa bila nyumba wala bandari. 1 Kuanzia nchi ya Kitimu + 23:1 Kitimu hapa ni Kipro, kisiwa katika Bahari ya Mediterania. 2 neno limewajia. 1