Acts 15:23
Wakatumwa na barua ifuatayo: Sisi mitume na wazee, ndugu zenu, Kwa ndugu Mataifa mlioamini mlioko Antiokia, Shamu na Kilikia: Salamu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Acts 14:27Walipowasili Antiokia wakaliita kanisa pamoja na kutoa taarifa ya yale yote Mungu aliyokuwa ametenda kupitia kwao na jinsi alivyokuwa amefungua mlango wa imani kwa ajili ya watu wa Mataifa.
Acts 15:4Walipofika Yerusalemu, walipokelewa na kanisa na mitume pamoja na wazee, ndipo Paulo na Barnaba wakawaarifu kila kitu Mungu alichokuwa amefanya kupitia kwao.
Acts 15:41Akapitia Shamu na Kilikia, akiimarisha makanisa ya huko.
Acts 21:3Tulipokiona kisiwa cha Kipro, tukakizunguka tukakiacha upande wetu wa kushoto, tukasafiri mpaka Shamu, tukatia nanga katika bandari ya Tiro ambapo meli yetu ilikuwa ipakue shehena yake.
Acts 23:26Klaudio Lisia, Kwa Mtawala, Mtukufu Feliksi: Salamu.
Galatians 1:21Baadaye nilikwenda sehemu za Syria + 1:21 Syria hapa ina maana ya Shamu. na Kilikia.