Acts 17:2
Kama desturi yake, Paulo aliingia ndani ya sinagogi, na kwa muda wa Sabato tatu akawa anahojiana nao kutoka kwenye Maandiko,
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Isaiah 1:18“Njooni basi tuhojiane,” 2 asema Bwana. 1 “Ingawa dhambi zenu ni kama rangi nyekundu, 2 zitakuwa nyeupe kama theluji; 1 ingawa ni nyekundu sana kama damu, 2 zitakuwa nyeupe kama sufu. 1
John 18:20Yesu akamjibu, “Nimekuwa nikizungumza waziwazi mbele ya watu wote. Siku zote nimefundisha katika masinagogi na Hekaluni, mahali ambapo Wayahudi wote hukusanyika. Sikusema jambo lolote kwa siri.
Acts 9:20Papo hapo akaanza kuhubiri kwenye masinagogi kwamba “Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu”
Acts 13:14Kutoka Perga wakaendelea hadi Antiokia ya Pisidia. Siku ya Sabato wakaingia ndani ya sinagogi, wakaketi.
Acts 17:10Usiku ule ule, wale ndugu walioamini wakawapeleka Paulo na Sila waende zao Beroya. Walipowasili huko wakaenda kwenye sinagogi la Wayahudi.
Acts 18:4Kila Sabato Paulo alikuwa akihojiana nao katika sinagogi, akijitahidi kuwashawishi Wayahudi na Wayunani.