Acts 17:29
“Kwa kuwa sisi ni watoto wa Mungu, haitupasi kudhani kuwa uungu ni kama sanamu ya dhahabu au ya fedha au ya jiwe, mfano uliotengenezwa kwa ubunifu na ustadi wa mwanadamu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 32:4Akavichukua vile vitu walivyomkabidhi, akavifanyiza kwa kusubu sanamu yenye umbo la ndama, akaichonga kwa kutumia chombo. Kisha wakasema, “Hii ndiyo miungu yenu, ee Israeli, iliyowapandisha kutoka Misri.”
Psalms 106:20Waliubadilisha Utukufu wao 2 kwa sanamu ya fahali, ambaye hula majani. 1
Isaiah 40:12Ni nani aliyepima maji ya bahari 2 kwenye konzi ya mkono wake, 2 au kuzipima mbingu kwa shibiri + 40:12 Shibiri ni sawa na sentimita 20 au inchi 8. yake? 1 Ni nani aliyeyashika mavumbi ya dunia katika kikapu, 2 au kupima milima kwenye kipimio 2 na vilima kwenye mizani? 1
Isaiah 44:9Wote wachongao sanamu ni ubatili, 2 navyo vitu wanavyovithamini havifai kitu. 1 Wale ambao wanazitetea ni vipofu, 2 ni wajinga, nao waaibika. 1
Jeremiah 10:4Wanaparemba kwa fedha na dhahabu, 2 wanakikaza kwa nyundo na misumari ili kisitikisike. 1
Romans 1:20Kwa maana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani, uweza wake wa milele na asili yake ya Uungu, imeonekana waziwazi, ikitambuliwa kutokana na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru.