Acts 23:11
Usiku uliofuata, Bwana akasimama karibu naye akamwambia, “Jipe moyo! Kama vile ulivyonishuhudia hapa Yerusalemu, hivyo imekupasa kunishuhudia huko Rumi pia.” 1 Hila Za Kumuua Paulo
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Psalms 46:1Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, 2 msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. 1
Isaiah 41:10Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe; 2 usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako. 1 Nitakutia nguvu na kukusaidia; 2 nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu. 1
Isaiah 43:2Unapopita kwenye maji makuu, 2 nitakuwa pamoja nawe, 1 unapopita katika mito ya maji, 2 hayatakugharikisha. 1 Utakapopita katika moto, 2 hutaungua, 2 miali ya moto haitakuunguza. 1
Jeremiah 15:19Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Kama ukitubu, nitakurejeza 2 ili uweze kunitumikia; 1 kama ukinena maneno yenye maana, 2 wala si ya upuzi, 2 utakuwa mnenaji wangu. 1 Watu hawa ndio watakaokugeukia, 2 wala si wewe utakayewageukia wao. 1
Matthew 14:27Lakini mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope.”
John 11:8Wanafunzi wake wakamwambia, “Rabi, Wayahudi walikuwa wanataka kukupiga mawe, nawe unataka kurudi huko?”