Acts 3:20
naye apate kumtuma Kristo, ambaye ameteuliwa kwa ajili yenu, yaani Yesu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
And he shall send Jesus Christ, which before was preached unto you:
In Context
Cross References
Matthew 16:27Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, naye ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Matthew 24:30“Ndipo itakapotokea ishara ya Mwana wa Adamu angani, na makabila yote ya dunia yataomboleza. Nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya angani, katika uwezo na utukufu mkuu.
Mark 13:30Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia.
Luke 21:27Wakati huo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni pamoja na uweza na utukufu mkuu.
2 Thessalonians 2:2msiyumbishwe kwa urahisi wala msitiwe wasiwasi na roho wala neno au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu, isemayo kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwako.
Hebrews 9:28vivyo hivyo Kristo alitolewa mara moja tu kuwa dhabihu ili azichukue dhambi za watu wengi. Naye atakuja mara ya pili, sio kuchukua dhambi, bali kuwaletea wokovu wale wanaomngoja kwa shauku.