Wakolosai 3:8
Lakini sasa yawekeni mbali nanyi mambo kama haya yote: yaani hasira, ghadhabu, uovu, masingizio na lugha chafu kutoka midomoni mwenu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
7Ninyi pia zamani mlienenda katika mambo haya mlipoishi maisha hayo.
9Msiambiane uongo, kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake,
Cross References
Psalms 37:8Epuka hasira na uache ghadhabu, 2 usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu. 1
Proverbs 19:19Mtu mwenye kukasirika haraka ni lazima atapata adhabu yake, 2 kama utamwokoa, itakubidi kufanya hivyo tena. 1
Matthew 5:22Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote atakayemkasirikia ndugu yake, atapaswa hukumu. Tena, yeyote atakayemwambia ndugu yake, ‘Raka,’ + 5:22 Raka ni neno la Kiaramu ambalo maana yake ni dharau au dhihaka ya hali ya juu. atapaswa kujibu kwa Baraza la Wayahudi. + 5:22 Baraza la Wayahudi lilikuwa kundi kuu kabisa la utawala wa Wayahudi lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu. Lakini yeyote atakayesema ‘Wewe mpumbavu!’ atapaswa hukumu ya moto wa jehanamu.
Romans 13:13Basi na tuenende kwa adabu kama inavyopasa wakati wa mchana, si kwa kufanya karamu za ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.
2 Corinthians 12:20Kwa kuwa nina hofu ya kwamba nitakapokuja naweza kuwakuta nisivyotaka, nanyi mkanikuta msivyotaka. Nina hofu kwamba panaweza kuwa na ugomvi, wivu, ghadhabu, fitina, masingizio, masengenyo, majivuno na machafuko.
Galatians 5:20kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,