Wakolosai 4:17
Mwambieni Arkipo hivi: “Hakikisha kuwa unakamilisha ile huduma uliyopokea katika Bwana.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 10:3Kisha Mose akamwambia Aroni, “Hili ndilo alilonena Bwana wakati aliposema: 1 “ ‘Miongoni mwa wale watakaonikaribia 2 nitajionyesha kuwa mtakatifu; 1 machoni pa watu wote 2 nitaheshimiwa.’ ” Aroni akanyamaza.
2 Chronicles 29:11Wanangu, basi msipuuze jambo hili sasa, kwa kuwa Bwana amewachagua ninyi msimame mbele zake na kumtumikia, mkawe watumishi wake na mkamfukizie uvumba.”
Matthew 25:17Yule aliyepewa talanta mbili akafanya vivyo hivyo, akapata nyingine mbili zaidi.
Acts 14:23Nao baada ya kuwateua wazee katika kila kanisa, kwa kufunga na kuomba wakawakabidhi kwa Bwana waliyemwamini.
1 Corinthians 4:1Basi, watu na watuhesabu sisi kuwa tu watumishi wa Kristo na mawakili wa siri za Mungu.
1 Timothy 4:6Kama ukiwakumbusha ndugu mambo haya, utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, uliyelelewa katika kweli ya imani na yale mafundisho mazuri uliyoyafuata.