Daniel 3:1
Mfalme Nebukadneza alitengeneza sanamu ya dhahabu, yenye kimo cha dhiraa sitini, + 3:1 Dhiraa sitini ni sawa na mita 27. na upana wa dhiraa sita, + 3:1 Dhiraa sita ni sawa na mita 2.7. akaisimamisha kwenye tambarare ya Dura katika jimbo la nchi ya Babeli.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 32:2Aroni akawajibu, “Vueni vipuli vya dhahabu ambavyo wake zenu, wana wenu na binti zenu wamevaa, mkaniletee.”
Deuteronomy 7:25Vinyago vya miungu yao mtavichoma moto. Msitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala msizichukue kwa ajili yenu, la sivyo mtakuwa mmetekwa navyo. Kwa kuwa ni chukizo kwa Bwana Mungu wenu.
1 Kings 12:28Baada ya kutafuta shauri, mfalme akatengeneza ndama wawili wa dhahabu. Akawaambia watu, “Ni gharama kubwa kwenu kukwea kwenda Yerusalemu. Hii hapa miungu yenu, ee Israeli, iliyowapandisha kutoka Misri.”
Esther 1:1Hili ndilo lililotokea wakati wa utawala wa Mfalme Ahasuero, yule aliyetawala juu ya majimbo mia na ishirini na saba tangu Bara Hindi hadi Kushi. + 1:1 Kushi hapa ina maana ya Ethiopia.
Psalms 135:15Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, 2 zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. 1
Isaiah 30:22Kisha mtanajisi sanamu zenu zilizofunikwa kwa fedha, na vinyago vyenu vilivyofunikwa kwa dhahabu. Mtazitupilia mbali kama vitambaa vya wakati wa hedhi na kuziambia, “Haya, tokeni hapa!”