Daniel 9:6
Hatukuwasikiliza watumishi wako manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, wakuu wetu, baba zetu, na watu wote wa nchi.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Chronicles 33:10Bwana akasema na Manase pamoja na watu wake, lakini hawakumjali.
2 Chronicles 36:16Lakini waliwadhihaki wajumbe wa Bwana wakayadharau maneno yake na kuwacheka manabii wake mpaka ghadhabu ya Bwana ikawa kubwa dhidi ya watu wake na hakukuwa na namna ya kuituliza.
Nehemiah 9:30Kwa miaka mingi ulikuwa mvumilivu kwao. Kwa njia ya Roho wako ukawaonya kupitia manabii wako. Hata hivyo hawakujali, basi ukawatia mikononi mwa mataifa jirani.
Nehemiah 9:34Wafalme wetu, viongozi wetu, makuhani wetu na baba zetu hawakufuata sheria yako. Hawakuzingatia amri zako wala maonyo uliyowapa.
Jeremiah 6:16Hivi ndivyo asemavyo Bwana: 1 “Simama kwenye njia panda utazame, 2 ulizia mapito ya zamani, 1 ulizia wapi ilipo njia nzuri, uifuate hiyo, 2 nanyi mtapata raha nafsini mwenu. 2 Lakini ninyi mlisema, ‘Hatutaipita hiyo.’ 1
Jeremiah 7:24Lakini hawakusikiliza wala kujali. Badala yake, walifuata ukaidi wa mioyo yao miovu. Walirudi nyuma badala ya kusonga mbele.