Kumbukumbu 4:20
Lakini kwenu ninyi, Bwana amewatoa kutoka kwenye tanuru ya kuyeyushia chuma, katika Misri kuwa watu wa urithi wake kama mlivyo sasa.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 19:5Sasa kama mkinitii kikamilifu na kutunza Agano langu, basi ninyi mtakuwa mali yangu ya thamani kubwa miongoni mwa mataifa yote. Ijapokuwa dunia yote ni mali yangu,
Deuteronomy 9:29Bali wao ni watu wako, urithi wako ule ulioutoa Misri kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyooka.”
1 Kings 8:51kwa maana ni watu wako na urithi wako, uliowatoa Misri, kutoka kwenye lile tanuru la kuyeyushia chuma.
Psalms 33:12Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, 2 watu ambao aliwachagua kuwa urithi wake. 1
Isaiah 63:17Ee Bwana, kwa nini unatuacha twende mbali na njia zako, 2 na kuifanya mioyo yetu migumu hata hatukukuheshimu? 1 Rudi kwa ajili ya watumishi wako, 2 yale makabila ambayo ni urithi wako. 1
Ephesians 1:18Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yatiwe nuru ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watakatifu