Mhubiri 2:8
Nikajikusanyia fedha na dhahabu, hazina za wafalme na za majimbo. Nikajipatia waimbaji wanaume na wanawake, nazo nyumba za masuria: vitu ambavyo moyo wa mwanadamu hufurahia.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Samuel 19:35Sasa nina miaka themanini. Je, naweza kutofautisha kati ya lililo jema na lililo baya? Je, mtumishi wako anaweza kujua ladha ya kile anachokula au anachokunywa? Je, bado naweza kusikiliza sauti za waimbaji wa kiume na za wanawake? Kwa nini mtumishi wako aongeze mzigo kwa bwana wangu mfalme?
1 Kings 9:28Wakasafiri kwa bahari mpaka Ofiri na kurudi na talanta 420 + 9:28 Talanta 420 za dhahabu ni sawa na tani 14. za dhahabu, ambazo walimkabidhi Mfalme Solomoni.
1 Kings 10:14Uzito wa dhahabu ambayo Solomoni alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666, + 10:14 Talanta 666 za dhahabu ni sawa na tani 25.
1 Kings 11:3Alikuwa na wake 700 mabinti wa uzao wa kifalme, na masuria 300, nao wake zake wakampotosha.
1 Kings 14:27Kwa hiyo Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba badala ya zile za dhahabu na kuzikabidhi kwa majemadari wa ulinzi wa zamu kwenye ingilio la jumba la mfalme.
1 Chronicles 25:6Hawa wanaume wote walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao kwa ajili ya uimbaji katika Hekalu la Bwana wakitumia matoazi, zeze na vinubi, kwa ajili ya huduma katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya usimamizi wa mfalme.