Esta 9:1
Katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, yaani mwezi wa Adari, amri iliyoagizwa na mfalme ilikuwa itekelezwe. Siku hii adui wa Wayahudi walikuwa wametumaini kuwashinda, lakini sasa mambo yaliwageukia na Wayahudi wakawashinda wale waliokuwa wanawachukia.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Samuel 22:41Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia, 2 nami nikawaangamiza adui zangu. 1
Esther 3:13Barua zilipelekwa na tarishi katika majimbo yote ya mfalme zikiwa na amri ya kuharibu, kuua na kuangamiza Wayahudi wote, wadogo kwa wakubwa, wanawake na watoto wadogo, siku moja, yaani siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari, na pia kuteka nyara vitu vyao.
Esther 9:17Hili lilitendeka siku ya kumi na tatu ya mwezi wa Adari na siku ya kumi na nne walipumzika na kuifanya siku ya karamu na furaha. 1 Kusherehekea Purimu
Psalms 30:11Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza, 2 ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe, 1
Isaiah 60:14Wana wa wale waliokuonea watakuja wakisujudu mbele yako, 2 wote wanaokudharau watasujudu kwenye miguu yako, 1 nao watakuita Mji wa Bwana, 2 Sayuni ya Aliye Mtakatifu wa Israeli. 1
Revelation 11:18Mataifa walikasirika nao 2 wakati wa ghadhabu yako umewadia. 1 Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa 2 na kuwapa thawabu watumishi wako manabii 1 na watakatifu wako pamoja na wale wote 2 wanaoliheshimu Jina lako, 2 wakubwa kwa wadogo: 1 na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.”