Ezekiel 11:21
Lakini kwa wale ambao mioyo yao imeambatana na vinyago vyao vya upotovu na sanamu zao za machukizo, nitaleta juu ya vichwa vyao yale waliyotenda asema Bwana Mwenyezi.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Jeremiah 1:16Nitatoa hukumu zangu kwa watu wangu 2 kwa sababu ya uovu wao wa kuniacha mimi, 1 kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine 2 na kuabudu kile ambacho mikono yao imekitengeneza.
Jeremiah 17:9Moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote, 2 ni mwovu kupita kiasi. 2 Ni nani awezaye kuujua? 1
Ezekiel 7:3Sasa mwisho umekuja juu yenu nami nitamwaga hasira yangu dhidi yenu. Nitawahukumu sawasawa na matendo yenu na kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za kuchukiza.
Ezekiel 9:10Kwa hiyo sitawahurumia wala kuwaachilia lakini nitaleta juu ya vichwa vyao, yale waliyoyatenda.”
Ezekiel 14:3“Mwanadamu, watu hawa wameweka sanamu katika mioyo yao na kuweka vitu viovu vya kukwaza mbele ya macho yao. Je, kweli niwaruhusu waniulize jambo lolote?
Ezekiel 20:31Mnapotoa matoleo yenu, yaani, wana wenu kafara katika moto, mnaendelea kujinajisi na sanamu zenu zote hadi siku hii ya leo. Je, niulizwe neno na ninyi, ee nyumba ya Israeli? Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, mimi sitaulizwa neno na ninyi.