Ezekieli 34:13
Nitawatoa katika mataifa na kuwakusanya kutoka nchi mbalimbali, nami nitawaleta katika nchi yao wenyewe. Nitawalisha kwenye milima ya Israeli, katika mabonde na mahali pote panapokalika katika nchi.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Psalms 106:47Ee Bwana Mungu wetu, tuokoe. 2 Tukusanye tena kutoka kwa mataifa, 1 ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu, 2 na kushangilia katika sifa zako. 1
Isaiah 49:9kuwaambia mateka, ‘Tokeni nje,’ 2 nao wale walio gizani, ‘Kuweni huru!’ 1 “Watajilisha kando ya barabara 2 na kupata malisho yao juu ya kila kilima kilicho kitupu. 1
Isaiah 66:19“Nitaweka ishara katikati yao, nami nitapeleka baadhi ya hao walionusurika kwa mataifa, hadi Tarshishi, kwa Puli + 66:19 Puli hapa inamaanisha Libya. na Waludi (wanaojulikana kama wapiga upinde), kwa Tubali na Uyunani, hadi visiwa vya mbali ambavyo havijasikia juu ya sifa zangu au kuuona utukufu wangu. Watatangaza utukufu wangu miongoni mwa mataifa.
Jeremiah 23:8bali watasema, ‘Hakika kama Bwana aishivyo, aliyewatoa wazao wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia,’ asema Bwana. Ndipo wataishi katika nchi yao wenyewe.” 1 Manabii Wasemao Uongo
Jeremiah 30:18“Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “ ‘Nitarudisha baraka za mahema ya Yakobo, 2 na kuhurumia maskani yake. 1 Mji utajengwa tena juu ya magofu yake, 2 nalo jumba la kifalme litasimama mahali pake halisi. 1
Jeremiah 32:37Hakika nitawakusanya kutoka nchi zote nilizowafukuzia katika hasira yangu kali na ghadhabu yangu kuu, nitawarudisha mahali hapa na kuwaruhusu waishi kwa salama.