Ezekieli 39:23
Na mataifa watajua kuwa nyumba ya Israeli walikwenda utumwani kwa ajili ya dhambi yao, kwa sababu hawakuwa waaminifu kwangu. Hivyo niliwaficha uso wangu na kuwatia mikononi mwa adui zao, nao wote wakaanguka kwa upanga.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
22Kuanzia siku ile na kuendelea nyumba ya Israeli itajua kuwa Mimi ndimi Bwana, Mungu wao.
24Niliwatendea sawasawa na uchafu wao na makosa yao, nami nikawaficha uso wangu.
Cross References
Deuteronomy 31:17Siku hiyo nitawakasirikia na kuwaacha; nitawaficha uso wangu, nao wataangamizwa. Maafa mengi na shida nyingi zitakuja juu yao, nao siku hiyo watauliza, ‘Je, maafa haya hayakuja juu yetu kwa sababu Mungu wetu hayuko pamoja nasi?’
Deuteronomy 32:20Akasema, “Nitawaficha uso wangu, 2 nami nione mwisho wao utakuwa nini, 1 kwa kuwa wao ni kizazi kilichopotoka, 2 watoto ambao si waaminifu. 1
Judges 2:14Hivyo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa wavamizi waliowateka nyara. Akawauza katika mikono ya adui zao pande zote, hivyo hawakuweza tena kuwazuia adui zao.
2 Chronicles 7:21Ingawa Hekalu hili linavutia sana sasa, wote watakaolipita watashangaa na kusema, ‘Kwa nini Bwana amefanya kitu kama hiki katika nchi hii na kwa Hekalu hili?’
Psalms 10:1Kwa nini, Ee Bwana, unasimama mbali? 2 Kwa nini unajificha wakati wa shida? 1
Psalms 106:41Akawakabidhi kwa mataifa 2 na adui zao wakawatawala. 1