Mwanzo 11:31
Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mwana wa Harani mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka kwa pamoja katika Uru ya Wakaldayo kwenda nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakaishi huko.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
30Sarai alikuwa tasa, hakuwa na watoto.
32Tera alikufa huko Harani akiwa na miaka 205.
Cross References
Genesis 11:26Tera alipokuwa na miaka sabini, akamzaa Abramu, Nahori na Harani. 1 Wazao Wa Tera
Genesis 12:4Hivyo Abramu akaondoka kama Bwana alivyokuwa amemwambia; naye Loti akaondoka pamoja naye. Wakati Abramu alipoitwa aondoke Harani, alikuwa na miaka sabini na mitano.
Genesis 14:12Pia walimteka Loti mwana wa ndugu yake Abramu pamoja na mali zake, kwa kuwa alikuwa akiishi Sodoma.
Genesis 24:10Ndipo huyo mtumishi akachukua ngamia kumi miongoni mwa ngamia za bwana wake, akaondoka, akiwa amechukua aina zote za vitu vizuri kutoka kwa bwana wake. Akaelekea Aramu-Naharaimu + 24:10 Yaani Mesopotamia ya Kaskazini-Magharibi. na kushika njia kwenda mji wa Nahori.
Genesis 27:43Sasa basi, mwanangu, fanya nisemalo: Kimbilia haraka kwa Labani ndugu yangu kule Harani.
Genesis 29:4Yakobo aliwauliza wachungaji, “Ndugu zangu, ninyi mmetoka wapi?” Wakamjibu, “Tumetoka Harani.”