Genesis 12:10
Basi kulikuwako na njaa katika nchi, naye Abramu akashuka kwenda Misri kukaa huko kwa muda, kwa maana njaa ilikuwa kali.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
9Kisha Abramu akasafiri kuelekea upande wa Negebu. 1 Abramu Katika Nchi Ya Misri
Cross References
Genesis 41:56Wakati njaa ilipokuwa imeenea katika nchi yote, Yosefu akafungua ghala za vyakula na kuwauzia Wamisri nafaka, kwa sababu njaa ilikuwa kali mno katika nchi yote ya Misri.
Genesis 42:5Hivyo wana wa Israeli walikuwa miongoni mwa wale waliokwenda Misri kununua nafaka, kwani njaa ilikuwa katika nchi ya Kanaani pia.
Genesis 46:3Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa baba yako, usiogope kushuka Misri, kwa maana huko nitakufanya taifa kubwa.
Ruth 1:1Wakati Waamuzi walipotawala Israeli, kulikuwa na njaa katika nchi. Mtu mmoja kutoka nchi ya Bethlehemu ya Yuda, pamoja na mke wake na wanawe wawili, akaenda kuishi katika nchi ya Moabu.
1 Kings 17:1Basi Eliya, Mtishbi kutoka Tishbi katika Gileadi, akamwambia Ahabu, “Kama Bwana, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninamtumikia, hapatakuwa na umande wala mvua katika miaka hii, isipokuwa kwa neno langu.”
2 Kings 6:25Kukawa na njaa kuu katika mji. Samaria ilizingirwa kwa muda mrefu, kiasi kwamba kichwa cha punda kiliuzwa kwa shekeli themanini + 6:25 Shekeli 80 za fedha ni sawa na kilo moja. za fedha, na robo ya kibaba + 6:25 Robo ya kibaba ni sawa na lita 0.3. cha mavi ya njiwa kiliuzwa kwa shekeli tano + 6:25 Shekeli tano za fedha ni sawa na gramu 55. za fedha.