Genesis 17:16
Nitambariki na hakika nitakupatia mwana kwake. Nitambariki na kwamba atakuwa mama wa mataifa, wafalme wa mataifa watatoka kwake.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 1:28Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.”
Genesis 15:4Ndipo neno la Bwana lilipomjia: “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako, bali mwana atakayetoka katika viuno vyako mwenyewe ndiye atakayekuwa mrithi wako.”
Genesis 18:10Kisha Bwana akasema, “Hakika nitakurudia tena majira kama haya mwakani na Sara mkeo atakuwa ana mwana.” Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema, lililokuwa nyuma yake.
Genesis 24:60Wakambariki Rebeka, wakamwambia, 1 “Ndugu yetu, uwe wewe kumi elfu, 2 mara elfu nyingi, 1 nao wazao wako wamiliki 2 malango ya adui zao.”
Isaiah 49:23Wafalme watakuwa baba zenu wa kuwalea, 2 na malkia wao watakuwa mama zenu wa kuwalea. 1 Watasujudu mbele yako nyuso zao zikigusa ardhi; 2 wataramba mavumbi yaliyo miguuni mwako. 1 Ndipo utajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana; 2 wale wanaonitumaini mimi hawataaibika.” 1
Galatians 4:26Lakini Yerusalemu wa juu ni huru, nayo ndiye mama yetu.