Genesis 18:30
Ndipo akasema, “Bwana na asikasirike, lakini niruhusu nizungumze. Je, kama huko watakuwepo thelathini tu?” Akajibu, “Sitapaangamiza ikiwa nitawakuta huko watu thelathini.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Judges 6:39Kisha Gideoni akamwambia Bwana, “Usinikasirikie. Ninaomba nifanye ombi moja lingine. Niruhusu nifanye jaribio jingine moja kwa ngozi hii. Wakati huu uifanye ngozi hii kavu na ardhi yote ifunikwe na umande.”
Job 40:4“Mimi sistahili kabisa: ninawezaje kukujibu wewe? 2 Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu. 1
Psalms 10:17Unasikia, Ee Bwana, shauku ya wanaoonewa, 2 wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao, 1
Isaiah 6:5Ndipo nikalia, “Ole wangu! Nimeangamia! Kwa kuwa mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninaishi katikati ya watu wenye midomo michafu, nayo macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana Mwenye Nguvu Zote.”
Hebrews 12:28Kwa hiyo, kwa kuwa tunapokea ufalme ambao hauwezi kutetemeshwa, basi na tuwe na shukrani, na hivyo tumwabudu Mungu kwa namna inayompendeza, kwa unyenyekevu na uchaji,