Mwanzo 28:14
Uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi na mashariki, kaskazini na kusini. Kupitia wewe na uzao wako mataifa yote ya duniani yatabarikiwa.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 12:3Nitawabariki wale wanaokubariki, 2 na yeyote akulaaniye nitamlaani; 1 na kupitia kwako mataifa yote duniani 2 yatabarikiwa.”
Genesis 13:16Nitaufanya uzao wako uwe mwingi kama mavumbi ya nchi, hivyo kama kuna yeyote awezaye kuhesabu mavumbi, basi uzao wako utahesabika.
Genesis 22:18na kupitia uzao wako mataifa yote duniani yatabarikiwa, kwa sababu umenitii.”
Genesis 32:12Lakini umeshasema, ‘Hakika nitakufanya ustawi na kuufanya uzao wako kuwa mwingi kama mchanga wa baharini ambao hauwezi kuhesabika!’ ”
Exodus 32:13Wakumbuke watumishi wako Abrahamu, Isaki na Israeli, ambao uliwaapia kwa nafsi yako mwenyewe: ‘Nitawafanya uzao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa wazao wako nchi hii yote ambayo niliwaahidia, nayo itakuwa urithi wao milele.’ ”
Deuteronomy 12:20Bwana Mungu wenu atakapokuwa ameongeza nchi yenu kama alivyowaahidi, nanyi mkitamani nyama na mkisema, “Ningependa nyama,” hapo unaweza kula nyingi upendavyo.