Hebrews 6:7
Ardhi ile ipokeayo mvua inyeshayo juu yake mara kwa mara hutoa mazao yanayowanufaisha wale ambao kwa ajili yao yalimwa, nayo nchi hiyo hupokea baraka kutoka kwa Mungu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 27:27Kwa hiyo akamwendea akambusu. Isaki aliposikia harufu ya nguo zake, akambariki, akasema, 1 “Aha, harufu ya mwanangu 2 ni kama harufu ya shamba 2 ambalo Bwana amelibariki. 1
Deuteronomy 28:11Bwana atakupa kustawi kwa wingi, katika tunda la uzao wa tumbo lako, katika wanyama wachanga wa mifugo yako na katika mazao ya ardhi yako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwapa.
Psalms 65:9Waitunza nchi na kuinyeshea, 2 waitajirisha kwa wingi. 1 Vijito vya Mungu vimejaa maji 2 ili kuwapa watu nafaka, 2 kwa maana wewe umeviamuru. 1
Psalms 126:6Yeye azichukuaye mbegu zake 2 kwenda kupanda, huku akilia, 1 atarudi kwa nyimbo za shangwe, 2 akichukua miganda ya mavuno yake.
Isaiah 55:10Kama vile mvua na theluji 2 ishukavyo kutoka mbinguni, 1 nayo hairudi tena huko 2 bila kunywesha dunia 1 na kuichipusha na kuistawisha, 2 hivyo hutoa mbegu kwa mpanzi 2 na mkate kwa mlaji, 1
Hosea 10:12Jipandieni wenyewe haki, 2 vuneni matunda ya upendo usio na kikomo, 1 vunjeni ardhi yenu isiyolimwa; 2 kwa kuwa ni wakati wa kumtafuta Bwana, 1 mpaka atakapokuja 2 na kuwanyeshea juu yenu haki. 1