Waebrania 9:15
Kwa sababu hii Kristo ni mpatanishi wa agano jipya, ili kwamba wale walioitwa waweze kupokea ile ahadi ya urithi wa milele: kwa vile yeye alikufa awe ukombozi wao kutoka kwa dhambi walizozitenda chini ya agano la kwanza.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Isaiah 53:10Lakini yalikuwa ni mapenzi ya Bwana 2 kumchubua na kumsababisha ateseke. 1 Ingawa Bwana amefanya maisha yake 2 kuwa sadaka ya hatia, 1 ataona uzao wake na kuishi siku nyingi, 2 nayo mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake. 1
Matthew 19:29Kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu zake wa kiume au wa kike, baba au mama, watoto au mashamba kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi ya hayo, na ataurithi uzima wa milele.
Matthew 25:36nilikuwa uchi mkanivika, nilikuwa mgonjwa mkanitunza, nami nilikuwa kifungoni mkaja kunitembelea.’
Luke 18:18Mtawala mmoja akamuuliza Yesu, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”
Romans 3:24wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu.
Romans 5:8Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu.