Hosea 3:1
Bwana akaniambia, “Nenda, ukaonyeshe upendo wako kwa mke wako tena, ingawa amependwa na mwingine naye ni mzinzi. Mpende kama Bwana apendavyo Waisraeli, ingawa wanageukia miungu mingine na kupenda mikate mitamu ya zabibu kavu iliyowekwa wakfu.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 7:6Kwa kuwa wewe ni taifa takatifu kwa Bwana Mungu wako. Bwana Mungu wako amekuchagua wewe kutoka mataifa yote juu ya uso wa dunia kuwa watu wake, hazina yake ya thamani.
Judges 10:16Nao wakaiondoa hiyo miungu migeni katikati yao nao wakamtumikia Bwana. Naye akahuzunika kwa sababu ya taabu ya Israeli.
2 Kings 13:23Lakini Bwana akawarehemu na akawahurumia, akaonyesha kujishughulisha nao kwa sababu ya Agano lake na Abrahamu, Isaki na Yakobo. Hadi leo, hajawaangamiza wala kuwafukuza mbele zake.
Nehemiah 9:31Lakini kwa rehema zako kuu hukuwakomesha wala kuwaacha, kwa kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na rehema.
Psalms 123:2Kama vile macho ya watumwa 2 yatazamavyo mkono wa bwana wao, 1 kama vile macho ya mtumishi wa kike 2 yatazamavyo mkono wa bibi yake, 1 ndivyo macho yetu yamtazamavyo Bwana Mungu wetu, 2 mpaka atakapotuhurumia. 1
Isaiah 45:22“Nigeukieni mimi, nanyi mkaokolewe, 2 enyi miisho yote ya dunia; 1 kwa maana mimi ndimi Mungu, 2 wala hapana mwingine. 1