Isaiah 36:17
mpaka nije nikawapeleke katika nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai mpya, nchi ya mkate na ya mashamba ya mizabibu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 3:8Basi nimeshuka niwaokoe kutoka mkono wa Wamisri, niwatoe na kuwapandisha kutoka nchi hiyo, niwapeleke katika nchi nzuri na kubwa, nchi itiririkayo maziwa na asali, nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi.
Deuteronomy 11:12Ni nchi ambayo Bwana Mungu wenu anaitunza; macho ya Bwana Mungu wenu yanaitazama daima kutoka mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka.
2 Kings 18:9Mwaka wa nne wa Mfalme Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa saba wa Hoshea mwana wa Ela kutawala Israeli, Shalmanesa mfalme wa Ashuru alikwenda kuishambulia Samaria na kuuzunguka kwa majeshi.
2 Kings 24:11Nebukadneza mwenyewe akaupandia mji wakati maafisa wake walipokuwa wameuzunguka kwa jeshi.
Proverbs 12:10Mtu mwenye haki hujali mahitaji ya mnyama wake, 2 bali matendo ya huruma ya mwovu ni ukatili. 1