Isaya 44:25
“mimi huzipinga ishara za manabii wa uongo, 2 na kuwatia upumbavu waaguzi, 1 niyapinduaye maarifa ya wenye hekima, 2 na kuyafanya kuwa upuzi, 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 9:11Waganga hawakuweza kusimama mbele ya Mose kwa sababu ya majipu yale yaliyokuwa miilini mwao na juu ya miili ya Wamisri wote.
2 Samuel 15:31Basi Daudi alikuwa ameambiwa, “Ahithofeli alikuwa miongoni mwa washiriki wa shauri baya la Absalomu.” Ndipo Daudi akaomba, akisema, “Ee Bwana, geuza shauri la Ahithofeli kuwa ujinga.”
2 Samuel 17:23Ahithofeli alipoona kwamba shauri lake halikufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka kwenda nyumbani kwake kwenye mji wake. Akaiweka nyumba yake katika utaratibu, kisha akajinyonga mwenyewe. Hivyo akafa na akazikwa katika kaburi la baba yake.
1 Kings 22:22“ Bwana akauliza, ‘Kwa njia gani?’ “Akasema, ‘Nitakwenda na kuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.’ “ Bwana akasema, ‘Utafanikiwa katika kumshawishi. Nenda ukafanye hivyo.’
2 Chronicles 18:11Manabii wengine wote walikuwa wanatabiri kitu hicho hicho, wakisema, “Ishambulie Ramoth-Gileadi na uwe mshindi. Kwa kuwa Bwana ataitia mkononi mwa mfalme.”
Job 5:12Huipinga mipango ya wenye hila, 2 ili mikono yao isifikie ufanisi. 1