James 5:11
Kama mnavyojua, tunawahesabu kuwa wabarikiwa wale waliovumilia. Mmesikia habari za uvumilivu wake Ayubu na mmeona kile ambacho hatimaye Bwana alimtendea. Bwana ni mwingi wa huruma, na amejaa rehema.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 34:6Bwana akapita mbele ya Mose, akitangaza, “ Bwana, Bwana, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu,
1 Chronicles 21:13Daudi akamwambia Gadi, “Ninayo mahangaiko makubwa. Mimi na nianguke mikononi mwa Bwana kwa maana rehema zake ni kuu mno, lakini usiniache niangukie mikononi mwa wanadamu.”
Nehemiah 9:17Wakakataa kusikiliza na kushindwa kukumbuka miujiza uliyoifanya miongoni mwao. Wakawa na shingo ngumu, na katika uasi wao wakamchagua kiongozi ili warudi kwenye utumwa wao. Lakini wewe ni Mungu mwenye kusamehe, mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo. Kwa hiyo hukuwaacha,
Job 1:2Alikuwa na wana saba na binti watatu,
Job 2:10Akamjibu, “Unazungumza kama vile ambavyo mwanamke mpumbavu + 2:10 Mpumbavu hapa ina maana ya kupungukiwa maadili. yeyote angenena. Je, tupokee mema mikononi mwa Mungu, nasi tusipokee na udhia?” Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi katika kusema kwake. 1 Marafiki Watatu Wa Ayubu
Job 23:10Lakini anaijua njia niiendeayo; 2 akiisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. 1