Yeremia 23:4
Nitaweka wachungaji juu yao ambao watawachunga, nao hawataogopa tena au kutishwa, wala hatapotea hata mmoja,” asema Bwana. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 26:9“ ‘Nitawaangalia kwa upendeleo na kuwafanya mzae na kuzidisha idadi yenu, nami nitalishika Agano langu na ninyi.
Psalms 78:70Akamchagua Daudi mtumishi wake 2 na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo. 1
Jeremiah 3:14“Rudini, enyi watu msio waaminifu, kwa kuwa mimi ni mume wenu,” asema Bwana. “Nitawachagua ninyi, mmoja kutoka kwenye mji, na wawili kutoka kwenye ukoo, nami nitawaleta Sayuni.
Jeremiah 30:10“ ‘Hivyo usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, 2 usifadhaike, ee Israeli,’ 4 asema Bwana. 1 ‘Hakika, nitakuokoa kutoka mbali, 2 wazao wako kutoka nchi ya uhamisho wao. 1 Yakobo atakuwa tena na amani na usalama, 2 wala hakuna atakayemtia hofu. 1
Jeremiah 33:26basi nitawakataa wazao wa Yakobo na Daudi mtumishi wangu, na sitachagua mmoja wa wanawe kutawala juu ya wazao wa Abrahamu, Isaki na Yakobo. Kwa maana nitawarudisha kutoka nchi ya kutekwa kwao na kuwaonea huruma.’ ”
Ezekiel 34:23Nitaweka juu yao mchungaji mmoja, mtumishi wangu Daudi, naye atawachunga, atawachunga na kuwa mchungaji wao.