Yeremia 44:5
Lakini hawakusikiliza wala hawakujali, hawakugeuka ili kuuacha uovu wao, wala hawakuacha kufukiza uvumba kwa miungu mingine.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Chronicles 36:16Lakini waliwadhihaki wajumbe wa Bwana wakayadharau maneno yake na kuwacheka manabii wake mpaka ghadhabu ya Bwana ikawa kubwa dhidi ya watu wake na hakukuwa na namna ya kuituliza.
Psalms 81:11“Lakini watu wangu hawakutaka kunisikiliza; 2 Israeli hakutaka kunitii. 1
Isaiah 48:18Laiti ungesikiliza kwa makini maagizo yangu, 2 amani yako ingekuwa kama mto, 2 haki yako kama mawimbi ya bahari. 1
Jeremiah 11:8Lakini hawakusikiliza wala kujali. Badala yake, walifuata ukaidi wa mioyo yao miovu. Hivyo nikaleta juu yao laana zote za agano nililokuwa nimewaamuru wao kulifuata, lakini wao hawakulishika.’ ”
Jeremiah 11:13Mnayo miungu mingi kama miji mliyo nayo, ee Yuda, nazo madhabahu mlizozijenga za kufukizia uvumba huyo mungu wa aibu Baali ni nyingi kama barabara za Yerusalemu.’
Jeremiah 19:13Nyumba zilizoko Yerusalemu na zile za wafalme wa Yuda zitatiwa unajisi kama mahali hapa, Tofethi: yaani nyumba zote ambazo walifukiza uvumba juu ya mapaa yake kwa jeshi lote la angani, na kumimina dhabihu za vinywaji kwa miungu mingine.’ ”