John 21:17
Kwa mara ya tatu Yesu akamuuliza Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akahuzunika sana kwa kuwa Yesu alimuuliza mara ya tatu, “Unanipenda?” Akamjibu, “Bwana, wewe unajua yote, unajua ya kuwa ninakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha kondoo wangu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Kings 17:18Akamwambia Eliya, “Una nini dhidi yangu, ewe mtu wa Mungu? Umekuja ili kukumbushia dhambi yangu na kusababisha kifo cha mwanangu?”
1 Chronicles 29:17Ninajua, Mungu wangu, kwamba wewe huujaribu moyo na unapendezwa na unyofu. Vitu hivi vyote nimetoa kwa hiari na kwa moyo mnyofu. Nami sasa nimeona kwa furaha jinsi watu wako walioko hapa kwa hiari yao walivyokutolea wewe.
Psalms 7:8Bwana na awahukumu kabila za watu. 1 Nihukumu Ee Bwana, 2 kwa kadiri ya haki yangu, 1 kwa kadiri ya uadilifu wangu, 2 Ewe Uliye Juu Sana. 1
Jeremiah 17:10“Mimi Bwana huchunguza moyo 2 na kuzijaribu nia, 1 ili kumlipa mtu kwa kadiri ya mwenendo wake, 2 kwa kadiri ya matendo yake yanavyostahili.” 1
Matthew 25:40“Naye Mfalme atawajibu, ‘Amin nawaambia, kwa jinsi mlivyomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.’
Mark 14:72Papo hapo jogoo akawika mara ya pili. Ndipo Petro akakumbuka lile neno Yesu alikuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akavunjika moyo, akalia sana.