John 6:7
Filipo akamjibu, “Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili, + 6:7 Dinari 200 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 200; mshahara wa kibarua ulikuwa dinari moja kwa siku. hazitoshi kununua mikate ya kuwapa watu hawa ili kila mtu apate kidogo.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
6Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya.
8Mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akamwambia,
Cross References
2 Kings 4:43Mtumishi wake akamuuliza, “Nitawezaje kuandaa hii mbele ya watu mia?” Lakini Elisha akajibu, “Wape watu ili wale. Kwa maana hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Watakula na kusaza.’ ”
Mark 6:37Lakini Yesu akawajibu, “Ninyi wapeni chakula.” Wakamwambia, “Je, twende tukanunue mikate ya dinari 200 + 6:37 Dinari moja ilikuwa kama mshahara wa kibarua wa siku moja; hivyo dinari 200 ni sawa na mshahara wa siku 200. ili tuwape watu hawa wale?”