John 8:12
Kisha Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu yeyote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
13Mafarisayo wakamwambia, “Ushuhuda wako haukubaliki kwa kuwa unajishuhudia mwenyewe.”
Cross References
Job 33:28Alinikomboa nafsi yangu nisitumbukie shimoni, 2 nami nitaishi ili kuufurahia mwanga.’ 1
Psalms 49:19atajiunga na kizazi cha baba zake, 2 ambao hawataona kamwe nuru ya uzima. 1
Isaiah 9:2Watu wanaotembea katika giza 2 wameona nuru kuu, 1 wale wanaoishi katika nchi ya uvuli wa mauti, 2 nuru imewazukia. 1
Isaiah 49:6yeye asema: 1 “Je, ni jambo dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu 2 ili kurejeza makabila ya Yakobo, 2 na kuwarudisha wale Waisraeli niliowahifadhi? 1 Pia nitakufanya uwe nuru kwa ajili ya watu wa Mataifa, 2 ili upate kuleta wokovu wangu hata miisho ya dunia.” 1
Isaiah 60:1“Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja 2 na utukufu wa Bwana umezuka juu yako. 1
Malachi 4:2Bali kwenu ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mabawa yake. Nanyi mtatoka nje na kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka zizini.