Yoshua 22:25
Bwana ameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi, ninyi Wareubeni na Wagadi! Hamna fungu kwa Bwana.’ Kwa hiyo wazao wenu wanaweza wakawasababisha wazao wetu wakaacha kumcha Bwana.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Samuel 26:19Sasa mfalme bwana wangu na asikilize maneno ya mtumishi wake. Kama Bwana amekuchochea dhidi yangu, basi yeye na aipokee sadaka yangu. Lakini hata hivyo, kama ni wanadamu waliofanya hivyo, walaaniwe mbele za Bwana! Wao sasa wamenifukuza kutoka sehemu yangu katika urithi wa Bwana wangu wakisema, ‘Nenda ukatumikie miungu mingine.’
1 Kings 12:16Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme: 1 “Tuna fungu gani kwa Daudi? 2 Sisi hatuna urithi kwa mwana wa Yese. 1 Nendeni kwenye mahema yenu, ee Israeli! 2 Angalia nyumba yako mwenyewe, ee Daudi!” Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao.
1 Kings 14:16Naye atawaacha Israeli kwa ajili ya makosa ya Yeroboamu aliyoyatenda na kusababisha Israeli kuyatenda.”
Ezra 4:2wakamjia Zerubabeli na viongozi wa jamaa, nao wakasema, “Turuhusuni tuwasaidie kujenga, kwa sababu sisi tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi na tumekuwa tukimtolea dhabihu tangu wakati wa Esar-Hadoni mfalme wa Ashuru, aliyetuleta hapa.”
Psalms 16:5Bwana umeniwekea fungu langu na kikombe changu; 2 umeyafanya mambo yangu yote yawe salama. 1