Judges 6:13
Gideoni akajibu, “Ee Bwana wangu, kama Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametutokea? Yako wapi basi yale matendo yake makuu baba zetu waliyotusimulia juu yake waliposema, ‘Je, Bwana hakutupandisha kutoka Misri?’ Lakini sasa Bwana ametuacha na kututia katika mkono wa Midiani.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
12Malaika wa Bwana alipomtokea Gideoni, akamwambia, “ Bwana yu pamoja nawe, Ewe shujaa mwenye nguvu.”
Cross References
Genesis 25:22Watoto wakashindana tumboni mwake, akasema, “Kwa nini haya yanatokea kwangu?” Kwa hiyo akaenda kumuuliza Bwana.
Numbers 14:14Nao watawaambia wenyeji wa nchi hii jambo hili. Wao tayari wameshasikia kwamba wewe, Ee Bwana, upo pamoja na watu hawa, na kuwa wewe, Ee Bwana, umeonekana uso kwa uso, nalo wingu lako hukaa juu yao. Tena wewe unawatangulia kwa nguzo ya wingu mchana na kwa nguzo ya moto usiku.
Deuteronomy 30:17Lakini kama moyo wako ukigeukia mbali ukawa huna utii, kama umevutwa kuisujudia miungu mingine na kuiabudu,
2 Chronicles 15:2Akatoka ili kumlaki Asa na kumwambia, “Nisikilizeni, Asa na Yuda wote na Benyamini. Bwana yu pamoja nanyi mkiwa pamoja naye. Kama mkimtafuta, ataonekana kwenu, lakini kama mkimwacha yeye, naye atawaacha ninyi.
Psalms 44:1Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu, 2 baba zetu wametueleza 1 yale uliyotenda katika siku zao, 2 siku za kale. 1
Psalms 77:7“Je, Bwana atakataa milele? 2 Je, hatatenda mema tena? 1