Walawi 17:7
Hawatatoa kamwe dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi ambazo wamekuwa wakijifanyia nazo ukahaba. Hili litakuwa agizo la kudumu kwao na kwa ajili ya vizazi vijavyo.’
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 22:20“Mtu awaye yote anayemtolea mungu mwingine dhabihu isipokuwa Bwana, lazima aangamizwe.
Exodus 32:8Wamekuwa wepesi kugeuka na kuacha niliyowaamuru, na wamejitengenezea sanamu ya kuyeyusha yenye umbo la ndama. Wameisujudia na kuitolea dhabihu, nao wamesema, ‘Hii ndiyo miungu yenu, ee Israeli iliyokupandisha kutoka Misri.’ ”
Leviticus 3:17“ ‘Hii ni kanuni ya kudumu kwa vizazi vijavyo, popote muishipo: Msile mafuta yoyote ya mnyama wala damu.’ ”
Deuteronomy 31:16Kisha Bwana akamwambia Mose: “Unakwenda kupumzika na baba zako, nao watu hawa hivi karibuni watazini na miungu migeni ya nchi wanayoingia. Wataniacha na kuvunja Agano nililofanya nao.
2 Chronicles 11:15Naye akawa amechagua makuhani wake mwenyewe kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia sanamu za mbuzi na za ndama ambazo alikuwa ametengeneza.
Jeremiah 3:1“Kama mtu akimpa talaka mkewe, 2 naye akamwacha na akaolewa na mtu mwingine, 1 je, huyo mume aweza kumrudia tena? 2 Je, hiyo nchi haitanajisika kabisa? 1 Lakini umeishi kama kahaba na wapenzi wengi: 2 je, sasa utanirudia tena?” 4 asema Bwana. 1